Soko Kuu Huria litakavyosaidia kukuza biashara Afrika
MACHI 21,2018 bara la Afrika liliandika historia mpya kufuatia viongozi 44 wa nchi za Afrika waliohudhuria Kikao Kisicho cha kawaida cha viongozi wa Afrika (Extraordinary Summit) kusaini mkataba utakaoruhusu kufanyika kwa biashara huru barani humu (Intra-African Free Trade).
Kusainiwa huku kwa Makubaliano kunamaanisha kuwa Mkataba wa Soko Kuu Huria la Afrika(AfCFTA) litakuwa eneo kubwa la biashara ambapo lengo kuu la makubaliano hayo ni kuzileta nchi zote 55 za bara la Afrika katika eneo moja la biashara (Single Market) kwa lengo la kunyanyua biashara barani Afrika.
Soko la bidhaa la pamoja barani Afrika kwa kiasi kikubwa litaweza kusaidia kuinua biashara kwa nchi za Afrika kwa kiwango kikubwa hususani kwa wafanyabiashara wa mipakani ambapo asilimia kubwa ni wanawake na vijana.Kuwepo kwa soko la pamoja litasaidia kwa kiasi kikubwa viwanda vya Afrika kuweza kujiwekeza katika eneo moja la uzalishaji (Specialization) na hivyo kuwa shindani (Competitive) kimataifa.
Tanzania ili iweze kuwa mshiriki mzuri wa mkataba huu wa AFCFTA na uchumi wake kuweza kukua na kufikia nchi ya uchumi wa kati mwaka 2025 kunahitajika mazingira wezeshi ya miundombinu ya kiuchumi na biashara.Miundombinu hii ni kama vile mtandao mpana wa barabara za lami, umeme wa kutosha na imara, reli za kisasa, bandari zenye kina kirefu sambamba na mfumo madhubuti wa uondoaji na upakuaji mizigo bandarini sambamba na mfumo wa pamoja wa usajiri wa biashara (One Stop Centre) ili kuondoa urasimu.
Akizungumza hivi karibuni kwa njia ya Mtandao katika mjadala wa namna ya Tanzania itanufaikaje na Mkataba wa Soko Kuu Huria la Afrika(AfCFTA),Mkurugenzi wa Shirika la Liberty Sparks, Evans Exaud anasema mkataba huo,wa kuwa na soko la pamoja utasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza biashara za nchi za kiafrika na kufanya kuwepo kwa hali ya ushindani.Anasema soko hilo pia litawezesha kuwa kwa ajira baina nya vijana wa kiafrika kutokana na masoko kuwa mengi na kuingiliana. “Kuwepo kwa Mkataba wa soko huru ni moja ya suluhisho la kuwepo kwa umasikini ,kukuza elimu kuchochea ushindani,kukuza viwanda vyetu vya ndani napia kupongeza ufanisi katika bidhaa zinazozaliahwa Afrika.“Mfano kama nchi rwanda inakuwa kwa kasi sana na ni nchi ya 143 kati ya nchi 193 hivyo rwanda inachukua hatua kubwa licha ya kuwa na changamoto nyingi katika udogo wake lakini inafanya vizuri katika masuala ya biashara,”anasisitiza
Akizungumzia Changamoto,Exaud anasema changamoto kubwa iliyopo katika nchi nyingi ni ishu za visa ambapo watu wanakosa kuwa huru katika kufanya biashara zao hata mipakani,lakini kwa watanzania ni rahisi kwenda Afrika ya Kusini,Kenya na Uganda.Anasema kuna nchi ambayo kuna Changamoto ya visa ambapo inafanya raia wao kushindwa kuingiliana hadi wawe na visa za kusafiria lakini kwa nchi ya Tanzania imeweza kuleta manufaa makubwa kwa watu wake.”Miongoni mwa wanufaikaji wakubwa wa fursa hiyo no Vijana na wakina ambao wamekuwa wakifanya biashara maeneo ya mipakani ,”anasema Akitaka Changamoto nyingine ,anasema tiketi za Ndege nazo zimekuwa ni Changamoto kutokana na watu wachache ambao wanaweza kulipa bei ya juu ya tiketi ya ndege hii inafanya biashara za kiafrika kudorora.
Anasema uwepo mkubwa wa hiyo SAfcta ni kutengeneza soko kubwa la kiafrika katika urahisi wa kuvuka wa bidhaa na urahisi wa kuvuka wa huduma na urahisi wa watu kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine’’watu wetu wataenda kupata nafasi katika kupata kazi na kuvuka kwa urahisi kupata nafasi ya kufanya biashara au ajira,huku ishu ya Viwanda kwenda kushindana ndani ya nchi na nje ya nchi ,urahisi wa upatikanaji wa bidhaa zinapozalishwa nchi Moja kuingia nyingine,”anasema
Naye Mtafiti na Mshirika wa Miradi wa Shirika la Liberty Sparks, LS,Michael Kyande,anasema soko hilo litasaidia kuwafanya wafanyabiashara kufanya biashara vizuri kwani itakuwa inaonyesha changamoto ambazo wafanyabiashara wanazipata katika mipaka. “Hii itasaidia wafanyabiashara kufanya biashara zao na kutatua changamoto za biashara,hii itasaidai kuwafanya wafanyabiashara wanaofanya biashara katika mipaka kuweza kufanya biashara vizuri,”anasema.
Anasema Soko hilo litaweza kukua hadi kwa masoko ya nje na kufanya Viwanda kuzalisha bidhaa zenye ushindani wa hali ya juu na kuongeza pato la nchi.”Soko hili litakapoanza litakuwa na manufaa kwa nchi za Afrika na kufanya nchi hizo kujiongezea pato la taifa la ndani ya nchi Moja na nyingine kutokana na kuruhusu biashara zilizopo mipakani,”anasema. Anasema biashara za ndani kwa ndani kwa nchi za Afrika iko chini ukilinganisha na mataifa ya nje,hivyo tutakapopata fursa ya kuwa na soko hili itasaidia biashara kukua kutoka asilimia 70 hadi asilimia 79 na kufanya bara la afrika kuanza kukua lenyewe.
Statement: A Peaceful, Freer and Prosperous Africa can Defeat Coups- African Think Tanks