Have any question?
+255 736 164 141
[email protected]
RegisterLogin
DONATE
  • About Us
    • Our Story
    • What we do
    • Our People
    • Jobs & Internships
    • Annual Reports & Financials
    • FAQs
    • Contact
  • Projects
  • Training
    • Overview
    • Certifications
    • Upcoming Courses
    • Think Tank Shark Tank
    • FAQs
  • Grants + Awards
  • Forums
  • About Us
    • Our Story
    • What we do
    • Our People
    • Jobs & Internships
    • Annual Reports & Financials
    • FAQs
    • Contact
  • Projects
  • Training
    • Overview
    • Certifications
    • Upcoming Courses
    • Think Tank Shark Tank
    • FAQs
  • Grants + Awards
  • Forums
  • News+Analysis
  • Media
    • Books
    • Videos
    • Champions of Change
  • Events
  • Shop
  • Support us
  • News+Analysis
  • Media
    • Books
    • Videos
    • Champions of Change
  • Events
  • Shop
  • Support us

Economics>Market

Sekta ya uvuvi: masoko ya nje ya nchi yatakavyopaisha uchumi wa tanzania

  • Posted by Bakari Mahundu
  • Categories Economics>Market, Op-ed
  • Date January 13, 2023
  • Comments 0 comment

Sector Yenye Matumaini

Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu za uchumi nchini inayochangia katika Pato la Taifa na kuondoa umaskini. Sekta hii inajumuisha shughuli zote za uvuvi wa asili na ukuzaji wa viumbe maji kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisasa. Kwa mwaka 2022, sekta ya uvuvi ilikuwa kwa asilimia 2.5 na ilichangia silimia 1.8 ya pato la taifa. Takriban Watanzania milioni 4.5 wamepata ajira kupitia sekta ya uvuvi katika mnyororo mzima wa sekta hiyo huku ajira za moja kwa moja. Taribani wavuvi zikiwa 195,000 na wakuza viumbe vya majini 31,998 wamepokea ajira kutokana na sekta ya uvuvi.

Tanzania: Utajiri wa baharini

Tanzania kuna bahari, mito, maziwa ambayo yanaweza kutumika vizuri kwenye uvunaji wa viumbe maji watakaoweza kusafirishwa na kuuzwa kwenye masoko ya nje ya nchi kupitia soko huria la nchi wanachama. Kwa mwaka 2021/2022 meli 6 zilipatiwa vibali kwa ajili ya uvuvi mkubwa wa kibiashara ambapo meli 3 ni za nje ya nchi na 3 ni za wawekezaji wa ndani. Bado kuna fursa kubwa kwa wawekezaji wa ndani kulichangamkia soko hili kubwa;

Vijana wengi wa Kitanzania wanaona kufanya biashara nje ya nchi ni jambo lisilowezekana. Kwa kawaida ni ngumu kwa kijana aliyehitimu chuo na aliyepo mtaani kuzitazama fursa za nje ya nchi kwani wengi wanaamini ni kitu kigumu na kisichowezekana. Hivyo inapelekea vijana wengi wajasiriamali wadogo hata wakubwa kuwekeza nguvu nyingi nchini pekee bila kuwa na mawazo ya kuvuka mipaka na kuanzisha viwanda, makapuni nje ya Tanzania.

Ukosefu wa elimu mahususi juu ya uwekezaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi ni kikwazo kwa vijana wengi wa Kitanzania hasa walihitimu vyuo vikuu. Kwakuwa mfumo wa elimu unamtaka mwanafunzi ajue zaidi katika masomo ya darasani hii imefanya wanafunzi wengi wa vyuo kutojua mambo mengine ya kibiashara nje ya masomo. Mfano mwanafunzi anayechukua masomo ya Kiswahili na historia, ni ngumu kujihusisha na masomo ya biashara, namna ya kuanzisha kampuni nje ya nchi, namna ya kusafirisha bidhaa bandarini na kadharika. Hii inapelekea vijana kutojiingiza kwenye biashara zinazojumuisha Bara la Afrika.

Ahadi ya Eneo la Biashara Huria

Itakumbukwa mwaka 2021 serikali ya Tanzania iliridhia mkataba wa eneo huru la biashara bara la Afrika (AfCFTA) na hivyo kuwa nchi ya 41 kati ya nchi 55 za Kiafrika zilizoridhia mkataba huo utakaowezesha nchi wanachama kufanya biashara bila vikwazo vya ushuru wa forodha. Hatua hii ni ya kupongezwa na kama ikiwekewa mikakati Madhubuti basi tatizo la ajira nchini litapungua kwa kiasi kikubwa:

Tanzania imebarikiwa maziwa, mito na bahari ya Hindi ambazo zote kwa Pamoja zinaweza kutumika kimkakati kutumia fursa za ACfTA kuzalisha bidhaa zitokanazo na uchumi wa buluu na kuzisafirisha katika nchi za Kiafrika ambazo hazina bahari. Hii inaipa Tanzania fursa za kujiimarisha kwenye uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na uchumi wa buluu zikiwemo aina kadhaa za samaki.

Kifuatacho ni Kipi?

Wizara ya Mifugo na Uvuvi haina budi kueneza elimu kwa wahitimu wa vyuo vikuu juu ya fursa zilizopo kwenye sekta hiyo, huku ikiweka mkakati wa kuwawezesha kwa teknolojia za kisasa ( visimba) na mabwawa kwa ajili ya uzalishaji mkubwa na wenye tija kuweza kushindana kwenye soko hilo Afrika.

Pia kulifanya somo la uvuvi kama sehemu ya masomo kwenye mitaala yetu itawezesha vijana wengi kutambua fursa nyingi zilizomo kwenye uchumi wa buluu. Hii ina maana kuwa kama elimu ya uvuvi na bidhaa zitokanazo na bahari itatolewa kuanzia chini na vyuo vikuu basi vijana wanaohitimu vyuo vikuu watapata mwanga mkubwa wa nini cha kufanya kujiajiri kwenye uchumi wa buluu na usafirishaji wa bidhaa zitokanazo na uchumi wa buruu nje ya Tanzania Kwenda nchi zingine za Kiafrika.

Mabalozi wa Tanzania Uganda, Rwanda, Botswana hawana budi kuweka mikakati ya kutangaza utajiri wa bidhaa zitokanazo na uchumi wa buluu zilizopo nchini Tanzania. Hapa kuna haja ya ubalozi kufanya ushirikiano wa kimkakati na wizara za biashara, sayansi na kilimo katika nchi husika ili kuwezesha upatikanaji wa bidhaa sahihi zinazohitajika katika nchi hizo. Sambamba na hilo, kuna umuhimu wa ubalozi kuratibu ziara za kibiashara na uwekezaji kwa vijana wa Kitanzania wanaojihusisha na bidhaa zitokanazo na uchumi wa buluu ili wakajionee soko na uhitaji halisi wa bidhaa hizo katika nchi husika.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi itoe vibali vingi kwa wakati bila urasmu kwa vijana wa Kitanzania walio tayari kusafirisha bidhaa za zitokanazo na uchumi wa buluu Kwenda kwenye nchi husika. Kama vibali hivi vitatolewa kwa wakati na kwa mashariti nafuu na rahisi basi vijana wengi watajitokeza kuchangamkia fursa hii itakoyopaisha pato lao na taifa kwa ujumla.

Michezo, Muziki ni miongoni mwa vitu vinavyowakutanisha vijana wengi, kama wasanii na wanamichezo wakubwa nchini wakitumika kama mabalozi kwa kuwawezesha kutembelea nchi husika na kutangaza fursa zilizopo huko basi bila shaka tutashuhudia ongezeko la vijana wengi kujihusisha na usafirishaji wa bidhaa zitokanazo na uchumi wa buluu nje ya nchi.

Mwisho kuna umuhimu wa serikali kuwahusha wadau kwenye sekta ya uvuvi kufanya tafiti za kisayansi juu ya mbegu bora za viumbe maji zitakazoweza kuleta ushindani kwenye masoko ya nchi husika, hivyo ni lazima njia za kisasa za kufuga viumbe maji  zitumike ili kuleta uzalishaji wenye tija.

Picture credit:Fichuo

  • Share:
Bakari Mahundu

Previous post

Markets and Human Flourishing Nairobi Workshop
January 13, 2023

Next post

Soko Kuu Huria litakavyosaidia kukuza biashara Afrika
January 25, 2023

You may also like

pexels-mjombadii-1410071
Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?
May 6, 2025
Xi Ruto
Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments
May 2, 2025
pexels-kampus-8476605
East Africa Must Embrace Free Market Reforms Now
April 30, 2025

Leave A Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search

MOST POPULAR

February 25, 2021
What Kombe’s saying about Business Regulations.
Read More
August 20, 2024
Impact of Cross-Border Conflicts on Trade in the East African Community
Read More
September 29, 2021
Idea Club for Emerging Leaders, recap for Saturday discussion.
Read More
September 12, 2022
Kwanini Tulalamike? NHIF inaweza Kuendelea Kuwepo?
Read More

RESEARCH & REPORT

Land Rights to Women in Tanzania Report

Land Rights to Women in Tanzania Report

In many parts of Sub-Saharan Africa, women, despite being...

Improved Economic Freedom Report 2022.

Improved Economic Freedom Report 2022.

Introduction Fraser Institute report (2021), the index published in...

Trading Across Borders: Implications & Policy Recommendations in Tanzania 2022 report

Trading Across Borders: Implications & Policy Recommendations in Tanzania 2022 report

Tanzania achieved a lower-middle-income economy status in July 2020,...

Tanzania Tax Reform Proposal 2021-2022

Tanzania Tax Reform Proposal 2021-2022

The Government of Tanzania released a public notice to...

Starting Busines Report in Tanzania 2021-2022

Starting Busines Report in Tanzania 2021-2022

Doing Business measures aspects of business regulation affecting small...

Global Alcohol Strategic Report

Global Alcohol Strategic Report

This paper in response to combatting paternalistic lifestyle regulations...

FEATURED ANALYSIS

Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?

Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?

Keeping Pace with China’s Digital Blitzkrieg The global financial...

Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments

Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments

Charm Offensive in China Kenya’s President Ruto was busy...

East Africa Must Embrace Free Market Reforms Now

East Africa Must Embrace Free Market Reforms Now

  Growth towards Economic Freedom As East Africa aspires...

The Single African Market Won’t Work Without these Localized Moyale Moments.

The Single African Market Won’t Work Without these Localized Moyale Moments.

      By Musila Muoki Streamlining Border Trade...

East Africa’s Brightest Sectors Are Being Left Out of Credential Recognition Frameworks

East Africa’s Brightest Sectors Are Being Left Out of Credential Recognition Frameworks

    By Musila Muoki Mutual Recognition of Expertise...

Cross Border Agricultural Trade in Tanzania 2025 Report

Cross Border Agricultural Trade in Tanzania 2025 Report

Introduction Liberty Sparks is a research-oriented think tank committed...

Cross Border Mineral Trade in Tanzania

Cross Border Mineral Trade in Tanzania

Introduction Liberty Sparks is a research-driven think tank dedicated...

Cross Border Manufacturing Trade in Tanzania Report 2025

Cross Border Manufacturing Trade in Tanzania Report 2025

Introduction Liberty Sparks is a research-oriented think tank committed...

JOIN OUR NEWSLETTER

Stay connected with what our team is accomplishing; subscribe today and get the full report and updates, straight to your inbox, every month.
You may also receive information and direct marketing from us, but you may update your preferences at any time.

Liberty Sparks

  • Kunduchi, Mtongania
    Jiwe gumu Road
  • Dar es Salaam, Tanzania
  • T +255 736 164 141
Facebook Twitter Youtube Instagram Linkedin Google-plus-g

A Freer, Flourishing Society

About

  • Our Story
  • Our People
  • What we do
  • Jobs & Internships
  • Annual Reports & Financials
  • FAQs
  • Contact
  • Our Story
  • Our People
  • What we do
  • Jobs & Internships
  • Annual Reports & Financials
  • FAQs
  • Contact

Awards

  • Grants
  • Awards
  • FAQs
  • Grants
  • Awards
  • FAQs

Events

Training

  • Overview
  • Certifications
  • Upcoming Courses
  • Think Tank Shark Tank
  • FAQs
  • Overview
  • Certifications
  • Upcoming Courses
  • Think Tank Shark Tank
  • FAQs

COPYRIGHT © 2023 LIBERTY SPARKS

Login with your site account

Lost your password?

Not a member yet? Register now

Register a new account

Are you a member? Login now