Tafiti za hivi karibuni zimedhihirisha kwamba idadi kubwa ya raia wa Uingereza wana mtazamo finyu wa Ubepari. Na wengi wao kutoka mrengo wa kushoto wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na uongozi wa sasa chama cha Labour, wamejizatiti kuupindua. Jambo hilo litakuwa janga kwa sababu, kama Eamonn Butler anavyotoa hoja katika chimbuko hili la Ubepari, ni msingi wa ustawi wetu na uhuru wetu, ushirika na nguvu kubwa yenye kuleta mabadiliko katika jamii. Ukosoaji mwingi dhidi ya Ubepari umesimama kwenye misingi ya uelewa mbaya uliozoelekakuhusiana na Ubepari, baadhi ya yake hata ukitoka kwa wafuasi wa Ubepari. Kikiwa kimeandikwa katika lugha rahisi na kuchukulia kama msomaji ‘hana ufahamu wa awali’ wa uchumi, kitabu hiki huwasaidia wasomaji kushinda mikanganyiko hii. Kinaelezea asili ya mtaji – utengenezaji wake, uhifadhi na uharibifu – na dhima ya masoko na haki ya kumiliki mali katika kufanya Ubepari ufanikiwe. Toleo hili kwa lugha ya kiswahili limefanyiwa tafsiri na Elias Mutani, kupitiwa na Evans Exaud. Limechapishwa na taasisi ya Liberty Sparks chini ya uangalizi wa Mkurugenzi Mtendaji wake Evans Exaud.