Bidhaa 10 kupelekwa soko huru la biashara Afrika
SERIKALI imetangaza kuanzia Julai Mosi mwaka huu itaan- za kupeleka bidhaa 10 katika Soko Huru la Biashara Afrika amba- lo Tanzania ni mwa wanachama. Akizungumza jana wakati wa ki- kao na Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi saba za mwanzo zilizopewa kipaumbele cha kupeleka bidhaa kwenye soko hilo na kuwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo.«Tumeshakutana Januari na jana ni kikao chetu cha tatu kukutana na wadau wazalishaji wa viwanda na wafanyabiashara kuelimishanakuhusu kinachohitajika kwenye eneo huru la biashara Afrika.
“Tayari tumeshapata bidhaa ya kwanza itakayotangulia ambayo ni kahawa na hatutapeleka ikiwa ghafi, tutapeleka iliyokwishachakatwa,” al-isema Dkt. Kijai. Waziri Kijaji alitaja bidhaanyingine itakayopelekwa kwenye soko hilo kuwa ni marumaru zinazozalishwa hapa nchini na hadi sasa tayari Ser-ikali imeshajadiliana na wazalishaji ambao wako tayari kusafirisha.”Kuna bidhaa zingine bado tuna-jadiliana na wazalishaji sitaziweka wazi lakini kwa ujumla tuko tayari kuingia na bidhaa 10 kwenye soko hili Kuanzia Julai Mosi mwaka huu, tunaendelea kuelezana kinachohitaji-kana vitu vya kuzingatia kutoka kwa wazalishaji wetu wa ndani.
“Niwahakikishie wazalishaji wetu wa viwandani na wale wa bidhaa zingine kwamba Serikali iko tayari na vikao hivi ni endelevu tutaendelea kupeana taarifa na kama alivyosema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Su-luhu Hassan kwamba tusiwe wasin-dikizaji,” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Leodeger Ten-ga, aliomba serikali kupunguza au kuondoa kodi kwa malighafi zin-azotoka ne ya nchi kwa ajili ya ku-saidia uzalishaji wa bidhaa mbalim-bali nchini. “Lazima tuwe waangalifu sana kwa viwanda vyetu vya ndani, una-posema soko huru unaweza kukuta wewe unageuzwa soko la bidhaa za wenzako kama hukutengenezwa mazingira mazuri kwa watu wako wa ndani kuzalisha bidhaa nzuri na kwa bei nafuu,” alisema Tenga.
Alisema kikao hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwao kwa sababu wamepata fursa ya kuelezea changamoto zao katika mazingira ya biashara.”Imekuwa nafasi nzuri kwa wenve viwanda na wafanyabiashara kui-shukuru serikali kwa mambo mema ambayo imefanya ambayo yako mengi na kukumbushana mengine ambayo bado yanahitaji kufanyiwa kazi,” alisema.
Alisema changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili wafanya-biashara zimefanyiwa kazi na seri-kali licha ya chache kubaki ambazo waliomba zifanyiwe kazi kupitia waziri huyo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.
Statement: A Peaceful, Freer and Prosperous Africa can Defeat Coups- African Think Tanks