Liberty sparks yakutana tena na washiriki kikosi kazi
Mkurugenzi wa taasisi ya Liberty Sparks , ndugu Evans Exaud alikutana na kuongoza kikao cha kikosi kazi kilichofanyika mtandaoni Julai 21 2022. Kikao kiliwakutanisha washiriki wa kikosi kazi ambao pia ni wakurugenzi wa sera na wakurugenzi watendaji katika taasisi mbalimbali ambao ni ndugu Andrew Mahiga kutoka TPSF, ndugu Isack Msungu kutoka CTI, ndugu Hamad Hamad kutoka ZNCC, ndugu Mercy Ngowo kutoka TCCIA na ndugu Mwajuma Hamza kutoka PWCC.
Kikao kilipitia na kuboresha ripoti inayokwenda kwa jina la biashara za Mipakani ( Trading Across borders implications and policy recommendations in Tanzania report 2022) ambayo itazinduliwa mnamo agosti 16 2022.
Walitumia kikao pia katika kujadili na kuweka sawa ratiba na agenda mbalimbali zinazokusudiwa kufanyika katika siku ya uzinduzi wa ripoti hiyo, ikiwemo agenda ya ushiriki na ushirikishwaji wa taasisi za kiserikali katika uzinduzi wa ripoti hiyo.
Nia kubwa ni kuhakikisha kuwa mapendekezo Yaliyopatikana kutoka katika tafiti iliyofanyika na Dr Petro Magai na mapendekezo kutoka kwa wadau wa kikosi kazi yanapitishwa na kuboreshwa Ili kuleta Mapinduzi na tija kwenye biashara za Mipakani.
Kama taasisi, tunaamini ni wakati sahihi wa Tanzania kujiweka katika mazingira mazuri ya kibiashara, haswa biashara ya mipakani Ili kuweza kushindana kwenye soko la ushindani na kuvutia uwekezaji nchini.
Statement: A Peaceful, Freer and Prosperous Africa can Defeat Coups- African Think Tanks