Biashara za Mipakani na Mapinduzi ya Kiuchumi Tanzania
Katika kuendeleza jitahada za kuchangia kuleta jamii huru na yenye mafanikio na kuhakikisha umaskini unapungua kwa Kasi, Liberty Sparks kupitia mradi wa cross border trade, chini ya kampeni ja ujirani mwema, imefanikiwa kuendelea kutoa elimu na kufanya tafiti nchini Tanzania.
Liberty Sparks iliandaa na kufanya mafunzo katika mipaka mitano ambayo ni Mtukula, Lusumo, Kabanga, Tunduma na Namanga. Mafunzo haya yalijikita katika kutoa elimu ya biashara za mipakani na jinsi gani biashara hizi zinaweza kuchochea maendeleo na kupunguza umaskini nchini Tanzania.
Mafunzo yalihusisha utoaji wa elimu kwa wafanya biashara na wafanyakazi wa serikali juu ya namna tunaweza kurahisisha biashara za mipakani, ufahamu kuhusu soko huru la Africa (AFCTA), manufaa ya kutokuwa na vikwazo mipakani na kwa jinsi gani kutokuwepo kwa vikwazo mbalimbali vya kisera na visivyo vya kisera kutasaidia biashara na maendeleo katika uchumi, na namna Wanawake na vijana wanaweza kunufaika kwa ujumla.
Wakati wa mafunzo haya, tulibaini na kukusanya changamoto mbalimbali zinazotokea na kuwakumba wafanyabiashara za mipakani. Wakati wa majadiliano na maoni mbalimbali wataalamu wetu walipata nafasi ya kujifunza zaidi na kurekodi maudhui yatakayotumika katika kutengeneza video ya ujirani mwema. Wadau pia walitoa mapendekezo mbalimbali kama kutamani uwepo wa muunganiko ambao utasajili taasisi ndogondogo na kuwepo kwa ofisi maalum kwa ajili ya kutoa suluhu ya matatizo yanayowapata wanawake na wafanya biashara wengine mipakani nk.
Kwa ujumla, mafunzo haya kwa sehemu kubwa yamekuwa na mafanikio makubwa na kuendelea kujenga ukaribu kati ya wafanyabiashara na wafanyakazi wa serikali mipakani na kwa ukaribu huu tunaamini utakuwa mwanzo mzuri wa kupatikana kwa suluhu za changamoto nyingi zisizo za kisera na za kisera katika mipaka yote ya Tanzania.
Statement: A Peaceful, Freer and Prosperous Africa can Defeat Coups- African Think Tanks