Maendeleo katika Uhuru wa Kiuchumi Tanzania 2022
- Version
- Download 309
- File Size 904.74 KB
- File Count 1
- Create Date February 13, 2023
- Last Updated April 12, 2023
Maendeleo katika Uhuru wa Kiuchumi Tanzania 2022
Utangulizi
Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Fraser (2021), orodha iliyochapishwa ya Uhuru wa Kiuchumi Duniani inaonesha kiasi ambacho sera na taasisi za nchi husaidia katika kuongeza uhuru wa kiuchumi. Muundo wa kielezo cha uhuru wa kiuchumi duniani unaonesha kiasi cha uhuru wa kiuchumi katika maeneo makuu matano, ambayo ni; Ukubwa wa Serikali; Mfumo wa Kisheria na Haki ya Kumiliki Ardhi; Uimara wa Sarafu; Uhuru wa Kufanya Biashara ya Kimataifa, na Udhibiti. Manufaa ya kiuchumi yanayoonekana wazi ya uhuru wa kiuchumi yamepelekea uwazi ulioongezeka kwenye biashara na mageuzi mengine yenye mwelekeo wa soko katika nchi zinazoendelea, katika iliyokuwa ngome ya Sovieti ya Ulaya Mashariki, na hata katika nchi zenye uchumi ulioendelea. Kielezi cha ripoti ya uhuru wa kiuchumi kimeiweka Tanzania katika fungu la tatu pamoja na nchi kama vile Kenya, Rwanda, Zambia, Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, na Namibia. Katika ripoti hii, Tanzania ilipata kiwango cha 6.75 na kushika nafasi ya 97 kati ya nchi 165. Katika Afrika kusini mwa Sahara, Tanzania inashika nafasi ya nane kati ya nchi 47 na kiwango chake cha jumla kipo juu ya wastani wa eneo hilo, ingawa kipo chini ya wastani wa dunia. Ripoti imesisitiza kwamba uhuru wa kiuchumi has matokeo makubwa katika kutokomeza umaskini na kuboresha ustawi wa Watanzania.
Lengo na Mbinu
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchanganua ripoti ya Taasisi ya Fraser iliyotolewa hivi karibuni ya “Orodha ya Nchi kwa Viwango vya Uhuru wa Kiuchumi Duniani”, na kufanya uchanganuzi kuchunguza “Kiwango cha Uboreshaji wa Uhuru wa Kiuchumi Tanzania 2021. Utafiti huu umetumia mbinu mchanganyiko za utafiti kufanya zoezi hili. Mbinu ya utafiti ya kupima ubora ilitumika kuchukua taarifa kutoka kwenye nyaraka sahihi na watoa taarifa waliochaguliwa. Katika zoezi hili, aina zote mbili za data; data msingi na data sekondari ziliochukuliwa na kuchanganuliwa. Vyanzo sekondari zilipatikana kimsingi kutoka kwenye uhakiki na uchanganuzi wa Orodha ya Nchi kwa Viwango vya Uhuru wa Kiuchumi Duniani ya mwaka 2021 iliyotolewa na Taasisi ya Fraser. Kwa lengo la utafiti huu, maeneo makuu manne ya uhuru wa kiuchumi yameangaliwa kikamilifu, ambayo ni; Mfumo wa Kisheria na Haki ya Kumiliki Ardhi, Uimara wa Sarafu, Uhuru wa Kufanya Biashara ya Kimataifa na Udhibiti. Utaratibu uliopelekea kukamilika kwa zoezi unahusisha kufanyika kwa majadiliano na kushirikisha taarifa husika zilizoainishwa kwenye michakato ya utayarishaji wa sera nchini Tanzania na kutoa uboreshaji wa hali ya juu viwango vya uhuru wa kiuchumi nchini Tanzania na mapendekezo ya sera kwa ajili ya kuwasilishwa kwa watunga sera.
Matokeo Makuu ya Utafiti
- Uelewa uliopatikana kupitia umeashiria kwamba uhuru wa kiuchumi hupelekea ukuaji wa kiuchumi na ustawi wa jamii. Hata hivyo, matokeo ya utafiti kuhusu uhusiano chanya baina ya uhuru na ukuaji wa kiuchumi na ustawi wa jamii yanaonesha mapungufu fulani. Maana yake ni kwamba ni sharti kuwe na vigezo vingine vya kuzingatia katika muktadha maalumu.
- Ufanisi wa Tanzania kuhusiana na mfumo wa kisheria na haki ya kumiliki ardhi uliendelea, kwa kiasi fulani, kubakia katika kiwango kilekile huku kiwango cha juu zaidi kikiwa nikikiwa ni 5.57 mwaka 2017 na kiwango cha chini zaidi kikiwa ni 5.3 mwaka 2019. Kiwango cha uhuru wa mahakama kilikuwa 5.29 na 5.4 mwaka 2018 na 2019 mtawalia. Hata hivyo, kulikuwa na kushuka kwa ujumla kwa Tanzania katika mfumo wa kisheria na haki ya kumiliki ardhi. Kushuka huko kwa sehemu fulani kulitokana na marekebisho ya sheria mbalimbali yaliyoshusha haki ya kumiliki ardhi kwa wamiliki wa ardhi. Pia ilipelekea kushuka kwa uhuru katika mfumo wa mahakama, kamapale ambapo serikali kama mihimili wa dola ulitwaa madaraka makubwa na kuipuuza mihimili mingine katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2020. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2020 kulikuwa na kasi ya kushuka kwa hali ya kuheshimu katiba au sheria kama ilivyoonekana kwa kuwafukuza kazi watumishi wa ngazi za juu serikalini katika mikutano ya hadhara kinyume na sheria ya utumishi wa umma na orodha ndefu ya makosa yasiyo na dhamana chini ya Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu iliyotumiwa katika kesi dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa serikali na waandishi wa habari wenye kuikosoa serikali.
- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakataza aina zote za ubaguzi. Haki za wanawake zimethibitishwa kikatiba lakini hazilindwi kwa ulinganifu. Licha ya kuwepo kwa sheria hizi za moja kwa moja, ikiwemo sheria mama inayolinda haki za wanawake chini Tanzania, bado kuna changamoto zinazowakabili wanawake. Idadi kubwa kiasi ya wanawake hawana uwezo wa kufanikisha haki yao ya kumiliki ardhi na mali nyingine kutokana na ukosefu wa uelewa wa sheria hizi na changamoto za utekelezaji wake. Kikwazo kikuu cha haki ya wanawake ya kumiliki ardhi ni kuwepo kwa sheria za mila, mazoea, desturi za urithi, mila na desturi zinazowanyima wanawake haki ya kumiliki mali.
- Kiwango katika uimara wa sarafu kimekuwa kizuri kwa zaidi ya 9.0. Mikopo iliyotolewa kwa sekta binafsi unaridhisha. Dalili ya kudumishwa kwa sera jumuishi ya fedha na kuboresha mazingira ya kufanya biashara. Mfumuko wa bei umekuwa umedhibitiwa kama inavyoonekana katika kiwango chake na kiasi kinachokubalika cha kupanda na kushuka.
- Mabenki na taasisi za fedha zinaruhusiwa to kutoa huduma ya fedha za kigeni kwa wakazi kuhusiana na malipo yote ya ya ndani na kigeni na jambo hili limebaki katika kiwango cha juu katika kipindi cha 2015-2019 kwa sababu katika kipindi hicho hapakuwa na mabadiliko yoyote katika udhibiti wa Serikali unaohusiana na umiliki na uendeshaji wa akaunti za benki katika fedha za kigeni.
Kumekuwa na kiwango cha chini cha mabadiliko katika uhuru wa kufanya biashara ya kimataifa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2019. Hii ni dalili ya uimara wa sera ya serikali katika kanuni zinazosimamia biashara ya kimataifa. Hata hivyo, kiwango cha mapato yatokanayo na kodi inayotozwa katika biashara kilishuka sana kutoka 8.82 mwaka 2015 hadi 7.34 mwaka 2019. Matokeo ya utafiti yalionesha, Tanzania ilifanya vibaya sana katika usimamizi wa vikwazo vya biashara na udhibiti, kiwango chake kikiwa 2.91 mwaka 2019, ambacho kilikuwa cha chini kuliko wastani
- Vikwazo visivyokuwa vya kifedha (NTBs) katika biashara vilifikia kiwango cha 4.82 mwaka 2016 kikipanda hadi 5.03 mwaka 2019 wakati ambapo gharama za lazima za kuagiza bidhaa/huduma toka nje na kuuza nje bidhaa/huduma zilibaki katika kiwango chake cha 0.80. Soko la biashara za magendo lilibaki katika kiwango chake cha 10.00 kipindi chote cha mwaka husika. Hii ilikuwa vivyohivyo katika uhuru wa wageni kutembelea Tanzania.
- Katika masharti ya mikopo, Tanzania ni ni nchi ya 58. Hii inamaanisha kwamba wafanyabiashara na wajasiriamali wanapitia ugumu usio wa lazima katika kupata mikopo kuanzisha au kutanua biashara na kutengeneza ajira na ustawi. Tanzania ilishika nafasi ya 13 kati ya nchi 15 kutoka Afrika kusimi mwa Sahara katika urahisi wa kupata mikopo. Kama soko linaloibuka, miradi mingi ya kibiashara nchini Tanzania imehangaika na uwezekano mgumu wa kupata mikopo, na asilimia 70 ya biashara zote za kati na ndogo nchini Tanzania, hazina uwezekano rasmi wa kupata mikopo kabisa. Kwa kweli, ni asilimia 15 tu ya watu wote ndio wenye uwezekano rasmi wa kupata mikopo kupitia mabenki.
- Ukosefu wa mikopo haumaanishi kwamba Watanzania siyo wakopaji wa fedha, kwa kuwa zaidi ya nusu ya wale waliopo katika katika soko la nguvukazi wamewahi kuchukua mikopo wakati fulani. Watanzania wengi wanatumia huduma za kifedha kupitia simu za mkononi.
- Uchanganuzi wa ufanisi wake kupitia Taasisi ya Fraser umeashiria kwamba, kiwango cha udhibiti wa soko la mikopo mwaka 2017 kilikuwa 7.84, ambapo kiasi hicho kiliongezeka kwa 0.32 mwaka 2018 hadi 8.18, kiwango hicho kilibaki katika ufanisi wake uleule mwaka 2019. Kiwango kinaonekana hivyo kwa sasa. Kufuatia janga la korona, Benki Kuu ya Tanzania iliendelea kuchukua mlolongo wa hatua za kisera kuitegemeza sekta ya kibenki, ikiwemo kushusha kiwangocha cini cha riba kutoka 7.0% hadi 5.0% na kupunguza kiwango cha chini cha uwiano wa mali kutoka 7.0% hadi 6.0% rasmi rasmi kuanzia 8 Juni 2020, ili kuchochea kuimarika kwa ufanisi wa soko. Licha ya mdororo wa dunia katika mikopo ya kifedha na ukuaji mwaka 2020 kutokana na UVIKO-19, sekta ya kibenki nchini Tanzania lilendelea kuimarika katika kiwango chake cha 4.1% kwa mwaka. huduma za kibenki kwa njia ya kidijitali zinaendelea kutanuka zikichochewa na kukua kwa ujumuishwaji wa kiuchumi na kiwango cha kuenea kwa matumizi ya simu za mkononi.
- Matokeo ya utafiti kuhusu ufanisi wa udhibiti wa kiwango cha riba (viwango hasi vya riba halisi) kyanaonyesha kwamba Tanzania iliweza kudhibiti riba katika kiwango kisichobadilika kutoka 2015 hadi 2017 kwa ufanisi wa 10 ukiporomoka taratibu hadi 9
- Wakazi wanafurahia kiasi fulani cha uhuru wa msingi unaofungamana na kusafiri na kubadili eneo la makazi, ajira, na elimu hasa wale wanaotoka katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati ambapo Itifaki ya Soko la Pamoja, inayohusisha uhamishaji huru wa nguvukazi, inatekelezwa ingawa siyo kikamilifu.
Mapendekezo
- Hapana budi kuchukua hatua ili kufikia viashiria vya msingi vya uhuru wa kiuchumi.
- Hali ya kuteleza iliyoonekana katika mwenendo kuhusiana na mfumo wa kisheria na haki ya kumiliki ardhi inastahili kutazamwa kwa umakini kwa kufanya uhakiki wa marekebisho yaliyofanyika katika sheria mbalimbali zilizoshusha haki ya kumiliki ardhi au kupelekea kushuka kwa uhuru katika mfumo wa mahakama.
- Haki ya wanawake kumiliki ardhi haina budi kuhimizwa kupitia ukuzaji wa kiwango cha uelewa wa sheria na uimarishaji wa mbinu za utekelezaji.
- Vikwazo vya kudhibiti biashara ambavyo vimekuwa vikali zaidi katika miaka mitano iliyopita havina budi kulegezwa.
- Ongeza kasi ya kufanya usimamizi wa kibenki kwa uangalifu zaidi na kuchochea tasnia madhubuti na kuendelea kutanua huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu na intaneti, ujumuishwaji wa kiuchumi na boresha mikopo kutoka sekta binafsi wakati huohuo punguza idadi ya mikopo inayosuasua.
- Udhibiti wa soko la nguvukazi hauna budi kuweka mizania kati ya kuwezesha mazingira bora ya kufanya kazi na vipato kwa waajiriwa.
- Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja, inayohusisha uhamishaji huru wa nguvukazi, hauna budi kuharakishwa na maendeleo yake kufanyiwa tathmini kwa kuzingatia uhuru wa msingi unaohusika.
Attached Files
File | Action |
---|---|
MAENDELEO KATIKA UHURU WA KIUCHUMI TANZANIA_compressed (1).pdf | Download |
1 Comment
Hello Liberty sparks!
I’m happy to join you, since I followed you im now refer myself as Economic freedom fighter under no violence of the law, thank so much for you good work all the time,