Have any question?
+255 736 164 141
[email protected]
RegisterLogin
DONATE
  • About Us
    • Our Story
    • What we do
    • Our People
    • Jobs & Internships
    • Annual Reports & Financials
    • FAQs
    • Contact
  • Projects
  • Training
    • Overview
    • Certifications
    • Upcoming Courses
    • Think Tank Shark Tank
    • FAQs
  • Grants + Awards
  • Forums
  • About Us
    • Our Story
    • What we do
    • Our People
    • Jobs & Internships
    • Annual Reports & Financials
    • FAQs
    • Contact
  • Projects
  • Training
    • Overview
    • Certifications
    • Upcoming Courses
    • Think Tank Shark Tank
    • FAQs
  • Grants + Awards
  • Forums
  • News+Analysis
  • Media
    • Books
    • Videos
    • Champions of Change
  • Events
  • Shop
  • Support us
  • News+Analysis
  • Media
    • Books
    • Videos
    • Champions of Change
  • Events
  • Shop
  • Support us

Op-ed

Mageuzi ya kilimo kupitia gmo: je, ni suluhu ya ukame na biashara ya kilimo afrika?

  • Posted by Ezra Nnko
  • Categories Op-ed
  • Date March 14, 2023
  • Comments 0 comment

Januari 1, 2021 yalisainiwa rasmi makubaliano ya utekelezaji wa mkataba wa eneo huru la biashara barani Afrika (AfCFTA). Shabaha  yake ni kukuza mashirikiano ya kibiashara baina ya nchi washirika kutoka 18% (sasa) hadi kufikia 52.3% kwa kuondoa ushuru wa forodha pamoja na kupunguza vizuizi visivyo na ushuru kwa bidhaa zaidi ya 60,000. Hatua hii inatarajiwa kukuza uchumi wa Afrika kufikia USD 29 trilioni ifikapo mwaka 2050.

Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) linaitaja Afrika, kama jumuiya yenye mchango mdogo zaidi duniani kwenye biashara ikichangia 2% tu. Kwa sasa jumla la pato zima la bara hilo ni USD Trilioni 3.4, hivyo kutekelezwa kwa mkataba huu kutaifanya pato likuwe kwa 7% kila mwaka. Kulingana na mapendekezo ya Kamisheni ya Uchumi wa Afrika (ECA), inaeleza moja ya mpango utakaofanikisha malengo haya kutimia ni uzidishaji wa bidhaa za kilimo.

Ikumbukwe; Mwaka 2003 ulisainiwa Mkataba wa Azimio la Maputo uliozitaka nchi wanachama wa AU kutenga 10% ya bajeti kuu ya matumizi kila mwaka kwa ajili ya Kilimo. Nchi nyingi zimekuwa  zikitenga kati ya 2-3%, hivyo kuifanya sekta ya kilimo kuendelea kudumaa. Mfano, mwaka 2020, ni nchi nne tu zikiwemo Malawi, Lesotho, Ethiopia na Benin) zilizotenga  bajeti yake kwa zaidi ya 10% kwenye kilimo

Hali hii inapelekea usalama wa chakula Afrika kuendelea kupungua. Ripoti ya Shirika la Biashara na Maendeleo Duniani (UNCTAD), ilieleza kuwa kati ya mwaka 2016-2018;   85% (thamani ya USD Bilioni 35 kwa mwaka) ya matumizi yote ya chakula Afrika iliagizwa kutoka Mataifa ya nje. Hivyo inakadiriwa kufikia mwaka 2025, uingizaji wa chakula kutoka nje utaongezeka na kufika USD Bilioni 110 kwa mwaka.

Ukiachilia mbali kiwango kidogo kinachotengwa kwenye bajeti ya Kilimo kwenye nchi nyingi za Afrika, pia kumekuwa na sababu mbalimbali zinazopelekea uzalishaji wa mazao ya kilimo kudorora. Sababu kama Matumizi duni ya teknolojia, Mabadiliko ya tabia nchi, elimu ya mabadiliko ya uzalishaji wa mazao, kukosekana kwa mnyororo wa uthaminishaji wa mazao ya kilimo n.k zimekuwa zikichochea sekta hii kushindwa kukua kwa kasi. Shirika la chakula Dunia (WFP), inaeleza kwa sasa watu Milioni 346 barani Afrika wanakabiliwa na upungufu wa chakula, zaidi chanzo ikiwa ni ukame.

Athari ya Ukame na uzalishaji mdogo wa Chakula unatazamiwa kuathiri hali ya Uchumi Afrika hasa kwenye ustawi wa watu kwenye lishe na gharama za upatikanaji wa bidhaa hizo, pia hali hiyo inatazamwa kutaathiri biashara ya mazao ya kilimo baina ya nchi washirika wa AfCFTA.

 

Mbegu za Uhandisi Jeni (GMO) ni Suluhisho la Ukame; Chakula na Biashara barani Afrika?

Tarehe 3, Oktoba 2022 serikali ya Kenya iliondoa katazo la Utafiti, Uzalishaji na Uingizaji wa mazao yanayotokana na mbegu za GMO. Katazo hili lililodumu kwa miaka 10, liliondolewa baada ya kuonekana kukua kwa ukame uliopelekea upungufu mkubwa wa chakula na maji. Ifahamike kuwa matumizi ya mbegu za GMO kwenye kilimo yameidhinishwa kwenye nchi 8 tu Afrika.

Kulingana na serikali ya Kenya; matumizi ya mbegu hizo yatapelekea ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula hasa ikitazamiwa mbegu hizi kuwa na uwezo mkubwa wa kuhimili ukame, kupambana na wadudu na pia kuongeza uzalishaji.

Kuchelea kwa mataifa mengi barani Afrika Pamoja na changamoto zake za chakula kupokea teknolojia hii; imechagizwa na maswali mengi ambayo baadhi ya tafiti zilizofanywa zimeonesha mbegu hizi kutokuwa suluhisho la changamoto ya uzalishaji wa mazao (hayo) pia kuonekana kuwa na athari kwenye afya ya binadamu na wanyama.

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Ndugu aliwahi kunukuliwa na gazeti moja la kila wiki akilinganisha uzalishaji wa pamba itokanayo na mbegu za GMO, ikionekana huzalisha 850 kg huku mbegu za kawaida (Hybrid and Open Pollinated) hukizalisha zaidi ya Tani 1.2-1.75 kwa ekari moja. Mpishano wa uzalishaji huo umeonekana pia kwenye mazao mengine, hivyo kuifanya mbegu hii kutokuonekana jawabu la uzalishaji mdogo.

National Center for Biotechnology Information ilielezea matumizi ya kemikali ya glyphosate ambayo hutumika kwenye utengenezaji wa mbolea ya mbegu ya GMO. Kemikali hiyo ilionekana kuleta athari kwenye viumbe ndani ya udongo na hivyo ili viumbe hivyo visipatwe na madhara hayo, vitahitajika vibadilishiwe uhandisi wa maumbile (GMO genetic engineering) ili viweze kupambana na mazingira. Hali hii itapelekea utegemezi wa teknolojia katika uzalishaji wa chakula ila pia kuharibu ikolojia asili ya viumbe hai.

Matumizi ya mbegu za GMO pia yameonekana kuathiri mazao yaliyo karibu, hasa ikizingatiwa kuwa mimea itokanayo na GMO ni mimea vamizi (invasive species) na hivyo inapotokea uchavishaji (Cross Pollination), mimea mingine inakuwa kwenye hatari ya kuharibika. Kwa hali hiyo, mbegu hizi zinaonekana kuweza kuathiri mimea na mazao mengine yasiyo na maumbile ya GMO, hivyo inalazimisha mimea yote kutengenezwa kwa mfanano wa maumbile ya GMO ili iweze kuishi. Jambo hili limeonekana kutishia uasili wa viumbe hai.

Taasisi ya Afya ya“The Lancet” ya Nchini Uingereza, ilifanya tafiti ya kuhusu vyakula vilivyozalishwa na mbegu ya GMO, tafiti hiyo ilionesha kuwa, mfano “Kiazi” ambacho kiliwekewa Bacillus Thuringiesis kama kemikali itakayotumika kukisaidia kupambana na wadudu.

Tafiti hiyo ilionesha endapo kama mwanadamu atakitumia atakuwa yupo hatarini kuathiriwa kiafya hasa uwezo wake wa kupambana na magonjwa, ukuaji wa chombo (organ), pamoja na mfumo wake wa mmengenyo wa chakula.

Pia kumekuwa na mkingamo wa umiliki wa teknolojia hii, hasa ikizingatiwa kuwa utengenezaji wa mbegu hizi hufanywa na taasisi binafsi; hali hii imeonekana italazimisha mataifa mengi kukabidhi haki ya upatikanaji wa chakula wa wananchi wao kwa taasisi binafsi. Suala hili linatazamwa kuathiri uhuru wa mwanadamu kwenye upatikanaji wa chakula.

Yapi Matokeo na Nini Kifanyike?

Mataifa mengi barani Afrika yameonekana kutokuwa tayari kupokea teknolojia hii. Hali hii itapelekea mataifa yaliyo idhinisha matumizi ya teknolojia hii kutokuwa na uwezo wa kuuza bidhaa hizo nje ya mipaka yao. Hatua hii itaathiri kwa kiwango kikubwa mashirikiano ya kibiashara ya chakula na mazao baina ya nchi washirika wa mkataba wa AfCFTA. Hatua hii inaweza kuwezesha mataifa hayo kujilisha pasipo kuwa msaada wa mataifa mengine.

Kwa kuwa shabaha ya mkataba wa AfCFTA ni kuondoa ushuru wa forodha ili kurahisisha muingiliano wa kibiashara na kuchagiza uchumi kukua. Mgawanyiko huu wa uzalishaji na ununuaji wa bidhaa ndani ya jumuiya ya nchi washirika vitachelewesha au kusababisha lengo hili lisifikiwe. Nchi za Afrika zinapaswa kuweka mkazo kwenye sera za kilimo na mnyororo wa bidhaa za kilimo.

Mataifa yenye hatari ya kupata ukame mara kwa mara yanapaswa kuweka mkazo kwenye kilimo cha umwagiliaji kwenye maeneo yasiyo na ukame na kujikita zaidi kwenye kilimo cha mazao yanayohimili ukame  ambayo pia yanaweza kuzalishwa kwa ziada na kuuzwa katika mataifa mengine. Mataifa haya yanapaswa kurudi na kutekeleza makubaliano ya Maputo kwani  tafiti zimeonesha  ustawi wa sekta ya kilimo baada ya kutenga bajeti ambayo itawezesha kufanyika kwa tafiti, usimamizi wa sera, uboreshaji wa miundombinu ya kilimo; utoaji wa elimu na ujuzi katika kilimo Pamoja na utoaji ruzuku kwenye bidhaa, zana, mbolea na pembejeo. Kama Afrika haitofikia makubaliano ya matumizi ya mbegu hizi, Mkataba wa AfCFTA utapungua manufaa. Afrika inapaswa kuamua.

Tag:#economics #market #afcfta

  • Share:
Ezra Nnko

Ezra Nnko is a Pan-Africanist, a Political and International Policy Analyst based in Tanzania. His work focuses much on analysing current affairs, economics, and social and international policies.

He can be available through: [email protected] or by mobile contact: +255b765 571917 / +255 784 527018

Previous post

Successful integrations for trade prosperity in africa.
March 14, 2023

Next post

Kahawa: Bidhaa ya kwanza kuipeleka AfCFTA. Tunaenda Kumuuzia Nani?
March 15, 2023

You may also like

whitman_Ndung_1100u
Trump’s Tariffs to Disrupt Kenya’s Growth
August 13, 2025
PAPSS-2
Currency Sovereignty as PAPSS Stakes Its Claim in Africa’s Currency Wars
July 2, 2025
pexels-michael-morse-1299434
Infrastructure Diplomacy in East Africa: The New Face of Regional Power and Influence
June 3, 2025

Leave A Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search

MOST POPULAR

February 25, 2021
What Kombe’s saying about Business Regulations.
Read More
August 20, 2024
Impact of Cross-Border Conflicts on Trade in the East African Community
Read More
September 29, 2021
Idea Club for Emerging Leaders, recap for Saturday discussion.
Read More
September 12, 2022
Kwanini Tulalamike? NHIF inaweza Kuendelea Kuwepo?
Read More

RESEARCH & REPORT

Land Rights to Women in Tanzania Report

Land Rights to Women in Tanzania Report

In many parts of Sub-Saharan Africa, women, despite being...

Improved Economic Freedom Report 2022.

Improved Economic Freedom Report 2022.

Introduction Fraser Institute report (2021), the index published in...

Trading Across Borders: Implications & Policy Recommendations in Tanzania 2022 report

Trading Across Borders: Implications & Policy Recommendations in Tanzania 2022 report

Tanzania achieved a lower-middle-income economy status in July 2020,...

Tanzania Tax Reform Proposal 2021-2022

Tanzania Tax Reform Proposal 2021-2022

The Government of Tanzania released a public notice to...

Starting Busines Report in Tanzania 2021-2022

Starting Busines Report in Tanzania 2021-2022

Doing Business measures aspects of business regulation affecting small...

Global Alcohol Strategic Report

Global Alcohol Strategic Report

This paper in response to combatting paternalistic lifestyle regulations...

FEATURED ANALYSIS

The Future of Microfinance Is Individual, Not Group-Based

The Future of Microfinance Is Individual, Not Group-Based

By Francis Nyonzo. The modern microfinance model, which uses...

Digital Payment as a Way to Increase the Freedom to Make Payments

Digital Payment as a Way to Increase the Freedom to Make Payments

By Francis Nyonzo   In my recently published paper...

Trump’s Tariffs to Disrupt Kenya’s Growth

Trump’s Tariffs to Disrupt Kenya’s Growth

With Donald Trump’s administration allowing a self-imposed trade deadline...

Currency Sovereignty as PAPSS Stakes Its Claim in Africa’s Currency Wars

Currency Sovereignty as PAPSS Stakes Its Claim in Africa’s Currency Wars

By Muoki Musila It’s a sovereignty issue… When I...

Infrastructure Diplomacy in East Africa: The New Face of Regional Power and Influence

Infrastructure Diplomacy in East Africa: The New Face of Regional Power and Influence

Why It Matters Kenya’s renewed plan to extend its...

If It Actually Works, Africa’s New Trade Route Could Be a Lifeline for Trade

If It Actually Works, Africa’s New Trade Route Could Be a Lifeline for Trade

By Muoki Musila   Hope in the Skies, but...

Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?

Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?

Keeping Pace with China’s Digital Blitzkrieg The global financial...

Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments

Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments

Charm Offensive in China Kenya’s President Ruto was busy...

JOIN OUR NEWSLETTER

Stay connected with what our team is accomplishing; subscribe today and get the full report and updates, straight to your inbox, every month.
You may also receive information and direct marketing from us, but you may update your preferences at any time.

Liberty Sparks

  • Kunduchi, Mtongania
    Jiwe gumu Road
  • Dar es Salaam, Tanzania
  • T +255 736 164 141
Facebook Twitter Youtube Instagram Linkedin Google-plus-g

A Freer, Flourishing Society

About

  • Our Story
  • Our People
  • What we do
  • Jobs & Internships
  • Annual Reports & Financials
  • FAQs
  • Contact
  • Our Story
  • Our People
  • What we do
  • Jobs & Internships
  • Annual Reports & Financials
  • FAQs
  • Contact

Awards

  • Grants
  • Awards
  • FAQs
  • Grants
  • Awards
  • FAQs

Events

Training

  • Overview
  • Certifications
  • Upcoming Courses
  • Think Tank Shark Tank
  • FAQs
  • Overview
  • Certifications
  • Upcoming Courses
  • Think Tank Shark Tank
  • FAQs

COPYRIGHT © 2023 LIBERTY SPARKS

Login with your site account

Lost your password?

Not a member yet? Register now

Register a new account

Are you a member? Login now