Have any question?
+255 736 164 141
[email protected]
RegisterLogin
DONATE
  • About Us
    • Our Story
    • What we do
    • Our People
    • Jobs & Internships
    • Annual Reports & Financials
    • FAQs
    • Contact
  • Projects
  • Training
    • Overview
    • Certifications
    • Upcoming Courses
    • Think Tank Shark Tank
    • FAQs
  • Grants + Awards
  • Forums
  • About Us
    • Our Story
    • What we do
    • Our People
    • Jobs & Internships
    • Annual Reports & Financials
    • FAQs
    • Contact
  • Projects
  • Training
    • Overview
    • Certifications
    • Upcoming Courses
    • Think Tank Shark Tank
    • FAQs
  • Grants + Awards
  • Forums
  • News+Analysis
  • Media
    • Books
    • Videos
    • Champions of Change
  • Events
  • Shop
  • Support us
  • News+Analysis
  • Media
    • Books
    • Videos
    • Champions of Change
  • Events
  • Shop
  • Support us

Op-ed

Kahawa: Bidhaa ya kwanza kuipeleka AfCFTA. Tunaenda Kumuuzia Nani?

  • Posted by Ezra Nnko
  • Categories Op-ed
  • Date March 15, 2023
  • Comments 0 comment

“Tayari tuna bidhaa ya kwanza tutakayoiuza nje, na bidhaa hiyo ni kahawa…hatotuoiuza ghafi bali tutauza kama bidhaa iliokamilika”. Alinukuliwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mh. Dk Ashatu Kijaji akiwaeleza wajumbe wa Shirikisho  la wenye Viwanda Tanzania (CTI)  juu ya uamuzi wa serikali kuisajili kahawa kama bidhaa ya kwanza kutoka Tanzania kwenye soko la biashara la eneo huru barani Afrika (AfCFTA). (Soma: https://allafrica.com/stories/202302140473.html).

Uamuzi huu ulifikiwa baada ya majadiliano ya miezi kadhaa baina ya serikali na wadau mbalimbali juu ya ipi iwe bidhaa ya kwanza kupelekwa kwenye soko la watu zaidi billioni 1.3.

Ikumbukwe Tanzania iliwasilisha uthibitisho wa kukubali uanachama na utekelezwaji wa mkataba huu (AfCFTA) mnamo tarehe 01 Januari 2021, hivyo iliweza kupata muda wa kutafiti na kujiandaa na ushindani pindi soko litakapofunguliwa.

Ukiachilia mbali Korosho na Tumbaku; Kahawa ni bidhaa ya kilimo ya tatu nchini yenye kuchangia pato kubwa ikikadiriwa mwaka 2021/22 kuchangia zaidi ya USD Millioni 142 baada ya mauzo. (Rejea: www.statista.com/statistics/1310392/value-of-agricultural-exports-from-tanzania na Hotuba ya Wizara ya Kilimo 2022/23, Uk 84).

Hali ya Kahawa Nchini (Uzalishaji).

90% ya wazalishaji wa kahawa nchini ni wakulima wadogo wadogo ambao huuza bidhaa zao kwa wafanyabiashara moja kwa moja au kupitia vyama vya ushirika. Serikali imekuwa ikijikita zaidi kwenye kuwawezesha wakulima kwenye elimu na uzalishaji hasa kwenye ugawaji wa miche, mbolea, dawa n.k pia usimamizi wa sera za soko na wataalamu hasa maafisa ugani.

Uzalishaji wa kahawa nchini umezidi kukua mwaka hadi mwaka; mfano mwaka (2017/18) uzalishaji ulikuwa tani 45,245, (2018/19) tani 68,147, (2019/20) tani 60,651, (2020/21) tani 73,027 na mwaka (2021/22) inakadiriwa kufika zaidi ya tani 65,235. Uzalishaji kwa mwaka 2019/20 ulipungua baada ya kuibuka kwa mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ulioathiri hali ya upatikanaji wa mahitaji ya uzalishaji hasa mbolea, pembejeo n.k ila pia mahitaji ya soko kupungua. (Rejea: Hotuba ya Wizara ya Kilimo 2022/23, Uk 91).

Serikali imekuwa ikiendelea kuweka mkazo kwenye uzalishaji; hasa ikitazamwa katika bajeti ya Wizara ya Kilimo 2022/23 ilitenga kiasi cha TZS Milioni 300 ambazo zingetumika katika uzalishaji na usambazaji wa miche bora 20,000,000 na kununua mashine mbili zenye uwezo wa kukaanga tani 15 za kahawa kwa saa, pia ukarabati wa mashamba, mafunzo ya kilimo bora,

uimarishaji wa masoko ikiwemo kuanzisha minada ya kahawa na kuratibu usimamizi wa mikataba ya ununuzi wa kahawa mfano mkataba wa AfCFTA).

Hali ya Soko la Kahawa

Ethiopia ni nchi ya kwanza barani Afrika na ya tano duniani kwa uzalishaji mkubwa na uuzaji wa kahawa ghafi ikikadiriwa kuuza zaidi ya tani 280,560 ikifuatiwa na Uganda ambayo mwaka 2022 kati 17%-19% ya fedha zote za kigeni zilipatikana kwenye mauzo ya kahawa. Nchi hizi mbili zimekuwa zikifanya biashara zaidi na mataifa kama Italia, Ujerumani, USA, Japan, Ubelgiji na mataifa ya Mashariki ya kati. (Rejea: U.S Foreign Agricultural Service, www.fas.usda.gov/data/ethiopia-coffee-annual-6 na https://www.fas.usda.gov/data/uganda-coffee-annual-6).

Nchini Uganda, serikali  imeonekana kujidhatiti kwenye uzalishaji na masoko; Kulingana na Mamlaka ya Maendeleo ya Kahawa nchini Uganda (UCDA), ustawi wa biashara hiyo itahitaji ongezeko la wanunuzi ambapo taasisi hiyo imelenga kupenya zaidi kwenye soko la China na mataifa ya Ulaya. Takwimu za mwaka 2021-2022 zilionesha Uganda ndio nchi pekee iliyowahi kupata kipato kikubwa kitokanacho na mauzo ya Kahawa ndani (ya mwaka mmoja) kwa kuuza bidhaa hiyo kwa thamani ya USD Milioni 862. (Rejea: Investment Monitor: https://www.investmentmonitor.ai/features/can-uganda-become-a-coffee-powerhouse).

Mataifa mengine yaliyojikita kwenye kilimo cha Kahawa barani Afrika ni Ivory Coast, Burundi, Rwanda na Kenya.

Kahawa Afrika? Tunamuuzia Nani?

Kama zilivyo nchi nyingi wazalishaji wa kahawa Afrika, Tanzania pia imekuwa ikiuza kahawa ghafi kwenye mataifa kama Japan, Italia na USA. Hali hii ya uuzaji wa kahawa katika mataifa haya ya nje ndio imepelekea taifa kuendelea kuwekeza zaidi kwenye kilimo hiki. Ripoti ya Tasnia ya Kahawa Tanzania: Mkakati wa Maendeleo 2011-2021, imeeleza kwa kina mpango wa ongezeko la uzalishaji kutoka wastani wa tani 50,000 hadi kufikia tani 100,000 mwaka 2021. Mpango huu kulingana na takwimu zilizooneshwa hapo juu kwa mwaka 2021 ni dhahiri zilishindikana kufikika.

Katika utekelezaji wa mkataba huu, moja ya njia ya kufikiwa malengo haya ni kuongeza mauzo kwenye mataifa washirika ya kibiashara hasa nchi kama Japan ambayo huchangia 15% ya mauzo ya bidhaa hii, Ujerumani, Italia na Ubelgiji (zote zikichangia 10%), huku 25% iliobakia ikipangwa kugawanywa kwenye nchi toauti tofauti hasa Finland na Switzerland.

Kulingana na Jukwaa la Uchumi Duniani, Afrika imekuwa na matumizi madogo ya kahawa ikilinganishwa na mataifa/jumuiya zingine duniani. Ukiachilia mbali taifa la Ethiopia ambao hupendelea kahawa ya “kwao” inayofahamika kama “ Yirgacheffe” ambapo kwa mwaka matumizi ya mtu mmoja ni kg 2.27,

mataifa mengine yamekuwa na utumiaji mdogo. Inakadiriwa nchi ya Algeria ni kg 3.2, Madagascar matumizi ni  kg 1, Ivory Coast kg 0.9 kwa mtu mmoja kwa mwaka, huku taifa kama la Brazil matumizi ni kg 6. Ripoti ya Euro Monitor ilielezea mataifa ya Ivory Coast na Uganda ambao ni wazalishaji wakubwa wa kahawa ingawa wananchi wake kwa wingi hutumia kakao na chai badala ya kahawa. Rejea: https://www.weforum.org/agenda/2015/10/which-african-countries-produce-the-most-coffee na https://www.emerald.com/insight/content/doi/10.1108/JHASS-03-2021-0046/full/html)

Kulingana na maelekezo ya Waziri Kijaji, Tanzania inapaswa kupeleka kahawa iliokamilika kama bidhaa na sio ghafi tena. Nchi nyingi za Afrika zimekuwa na utaratibu zinazoathiri uchumi wake kwa kutokuwekeza kwenye uendelezaji wa mnyororo wa bidhaa kwa kuziongezea thamani na kuziuza zikiwa ghafi. Bajeti ya Wizara ya Kilimo Pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara zinapaswa kuangalia ni kwa namna gani baadhi ya bidhaa tunazozitengeneza ziingizwe kwenye soko la ushindani ziweze kuongeza thamani kwenye uchumi wetu.

Pamoja na hayo, tafiti kubwa zifanyike kwenye chaguzi wa bidhaa kwenye soko la ushindani hasa mkataba wa AfCFTA unaotekelezwa sasa, kwani kwa bidhaa kama kahawa ambayo soko lake kubwa limekuwa kwenye mataifa ya nje, kuiweka kama bidhaa namba moja kwenye ushindani katika soko la AfCFTA inaweza isiwe na tija kwa kuwa sio bidhaa hitajika kwenye soko la Afrika.

Chaguzi ya bidhaa hizi pia zinapaswa kusindikizwa na mpango wa kuzilinda kwenye ushindani kupitia bajeti ya wizara na serikali kuu Pamoja na wataalam wa soko na ushawishi. Kiujumla uwekezaji katika ushindani  unapaswa kuzingatiwa.

Tanzania inaweza kuitumia fursa hii ya kuitangaza kahawa katika soko la AfCFTA, ili kupata uwekezaji wa viwanda ndani ya nchi kutokana na sheria ya mkataba ya “Rule of Origin”ambayo inahitaji bidhaa izalishwe ndani ya Afrika. Changamoto ni uwepo wa soko la kuhakikisha uwekezaji huu unalipa kwa mwekezaji na serikali kwa ujumla.

Ni wazi tutatambulisha bidhaa hii katika soko la AfCFTA, Julai 2023 lakini haitoweza kushindana na kuleta tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Tag:#economics #market #afcfta

  • Share:
Ezra Nnko

Ezra Nnko is a Pan-Africanist, a Political and International Policy Analyst based in Tanzania. His work focuses much on analysing current affairs, economics, and social and international policies.

He can be available through: [email protected] or by mobile contact: +255b765 571917 / +255 784 527018

Previous post

Mageuzi ya kilimo kupitia gmo: je, ni suluhu ya ukame na biashara ya kilimo afrika?
March 15, 2023

Next post

Christian Or Muslim, Free Enterprises and Property Right is the key to End Poverty.
March 23, 2023

You may also like

pexels-mjombadii-1410071
Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?
May 6, 2025
Xi Ruto
Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments
May 2, 2025
pexels-kampus-8476605
East Africa Must Embrace Free Market Reforms Now
April 30, 2025

Leave A Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Search

MOST POPULAR

February 25, 2021
What Kombe’s saying about Business Regulations.
Read More
August 20, 2024
Impact of Cross-Border Conflicts on Trade in the East African Community
Read More
September 29, 2021
Idea Club for Emerging Leaders, recap for Saturday discussion.
Read More
September 12, 2022
Kwanini Tulalamike? NHIF inaweza Kuendelea Kuwepo?
Read More

RESEARCH & REPORT

Land Rights to Women in Tanzania Report

Land Rights to Women in Tanzania Report

In many parts of Sub-Saharan Africa, women, despite being...

Improved Economic Freedom Report 2022.

Improved Economic Freedom Report 2022.

Introduction Fraser Institute report (2021), the index published in...

Trading Across Borders: Implications & Policy Recommendations in Tanzania 2022 report

Trading Across Borders: Implications & Policy Recommendations in Tanzania 2022 report

Tanzania achieved a lower-middle-income economy status in July 2020,...

Tanzania Tax Reform Proposal 2021-2022

Tanzania Tax Reform Proposal 2021-2022

The Government of Tanzania released a public notice to...

Starting Busines Report in Tanzania 2021-2022

Starting Busines Report in Tanzania 2021-2022

Doing Business measures aspects of business regulation affecting small...

Global Alcohol Strategic Report

Global Alcohol Strategic Report

This paper in response to combatting paternalistic lifestyle regulations...

FEATURED ANALYSIS

Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?

Will Africa’s PAPSS Survive the Coming Digital Currency Wars?

Keeping Pace with China’s Digital Blitzkrieg The global financial...

Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments

Kenya at the Crossroads of China, the U.S., and Africa amidst Global Tarde Realignments

Charm Offensive in China Kenya’s President Ruto was busy...

East Africa Must Embrace Free Market Reforms Now

East Africa Must Embrace Free Market Reforms Now

  Growth towards Economic Freedom As East Africa aspires...

The Single African Market Won’t Work Without these Localized Moyale Moments.

The Single African Market Won’t Work Without these Localized Moyale Moments.

      By Musila Muoki Streamlining Border Trade...

East Africa’s Brightest Sectors Are Being Left Out of Credential Recognition Frameworks

East Africa’s Brightest Sectors Are Being Left Out of Credential Recognition Frameworks

    By Musila Muoki Mutual Recognition of Expertise...

Cross Border Agricultural Trade in Tanzania 2025 Report

Cross Border Agricultural Trade in Tanzania 2025 Report

Introduction Liberty Sparks is a research-oriented think tank committed...

Cross Border Mineral Trade in Tanzania

Cross Border Mineral Trade in Tanzania

Introduction Liberty Sparks is a research-driven think tank dedicated...

Cross Border Manufacturing Trade in Tanzania Report 2025

Cross Border Manufacturing Trade in Tanzania Report 2025

Introduction Liberty Sparks is a research-oriented think tank committed...

JOIN OUR NEWSLETTER

Stay connected with what our team is accomplishing; subscribe today and get the full report and updates, straight to your inbox, every month.
You may also receive information and direct marketing from us, but you may update your preferences at any time.

Liberty Sparks

  • Kunduchi, Mtongania
    Jiwe gumu Road
  • Dar es Salaam, Tanzania
  • T +255 736 164 141
Facebook Twitter Youtube Instagram Linkedin Google-plus-g

A Freer, Flourishing Society

About

  • Our Story
  • Our People
  • What we do
  • Jobs & Internships
  • Annual Reports & Financials
  • FAQs
  • Contact
  • Our Story
  • Our People
  • What we do
  • Jobs & Internships
  • Annual Reports & Financials
  • FAQs
  • Contact

Awards

  • Grants
  • Awards
  • FAQs
  • Grants
  • Awards
  • FAQs

Events

Training

  • Overview
  • Certifications
  • Upcoming Courses
  • Think Tank Shark Tank
  • FAQs
  • Overview
  • Certifications
  • Upcoming Courses
  • Think Tank Shark Tank
  • FAQs

COPYRIGHT © 2023 LIBERTY SPARKS

Login with your site account

Lost your password?

Not a member yet? Register now

Register a new account

Are you a member? Login now