Waandishi wa habari waomba kuandika makala za uchumi, elimu, biashara na masoko
WAANDISHI wa habari na vijana wanaofanya tafiti katika masuala ya uchumi, elimu, biashara na Masoko wametakiwa kujikita katika kuandika makala mbalimbali zitakazolenga kuleta mapinduzi katika sekta hizo.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la COMALISO la nchini Zimbabwe Rejoice Ngwenya wakati wa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari na vijana watafiti iliyoandaliwa na Taasisi inayojihusisha na masuala ya elimu, utetezi na Masoko ya Liberty Sparks.
Ngwenya amesema uandishi wa makala ni kipaji kama vilivyo vipaji vingine hivyo vijana wasisite kuovionyesha kwa kuandika makala ambazo zitalenga kunisaidia jamii.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Liberty Sparks, Evans Exaud amesema ni muhimu pia vijana wakatambua masuala ya soko huria na kujenga jamii iliyohuru na yenye maendeleo.
Chanzo: 2eyesmedia
Statement: A Peaceful, Freer and Prosperous Africa can Defeat Coups- African Think Tanks