Kiini Cha Demokrasia
Demokrasia ni nini? Inafanya kazi namna gani? Ina uwezo gani thabiti – na yapi ni mapungufu yake?
Theluthi mbili ya watu duniani, katika zaidi ya nchi 100, wanaishi chini ya serikali zinazodai kuwa za kidemokrasia. Bado ni chache kati ya serikali hizo ndizo zinazoheshimu mifano bora kabisa ya demokrasia,au kuheshimu misingi yake mikuu pamoja na desturi zake.
Ndani ya kitabu hiki, mwandishi Eamonn Butler anatoa maana ya demokrasia, anaelezea lengo lake, na anaonesha tofauti kati ya demokrasia ya kweli na aina nyingi zilizopo za demokrasia ya ulaghai.
Anatoa kwa ufupi historia ya demokrasia na manufaa inayoleta. Lakini anaonesha pia mambo mengi dhanifu juu ya demokrasia, yanayofanya tushindwe kuona ukomo wake.
Na anaelezea kwa nini ni muhimu kuwa na uelewa bayana wa demokrasia na jinsi ilivyo rahisi kwa demokrasia kupotea au kutumiwa vibaya pale watu wanapokosa kujua maana yake kwa usahihi.
Kwa kutilia mkazo, anahoji kwa nini watu wengi leo hii wamevunjika moyo kutokana na siasa za kidemokrasia – na kama kuna chochote kinachoweza kufanyika kuhusu hali hiyo.
Kitabu hiki kinachoeleweka kwa urahisi na chenye kuvutia kinatoa usuli wa moja kwa moja wa demokrasia, na kumwezesha mtu yeyote kuielewa – hata kama hajapitia uzoefu wake.