Msingi wa Ujasiriamali
Wajasirimali wana jukumu lenye umuhimu wa kipekee katika kuchochea maendeleo, uwezo zalishi na ustawi.
Wanasukuma mbele ukuaji wa kiuchumi na kutengeneza fursa mpya.Uvumbuzi wao hubadili maisha ya watu, Mchango wao mkubwa haufahamiki kwa mapana yake na mara nyingi unapuuzwa na waandishi wa vitabu vya kiada.
Katika kitabu hiki, mwandishi Eamonn Butler,kinaugaubaga anaelezea jukumu kubwa la ujasiriamali, anachambua umhimu wake kiuchumi na kijamii, na kutathmini mazingira yanayohitajika kwa ajili ya Ujasiriamali kushamiri.
Ndani ya kitabu anatolea mifano ya watu “wasio wa kawaida” waliokuja kuwa wajasiriamali.Nani alikuwa anajua, kwa mfano kwamba Mark Zuckerberg wa Facebook, mwanzilishi wa Microsoft aitwaye Bill Gates, mwanzilishi mwenza wa Apple aitwaye Steve Jobs na Mwanzilishi wa Uber aitwaye Travis Kalanick wote walikatisha masomo ya chuo kikuu? Au kwamba mwanzilishi Virgin Group aitwaye Sir Richard Branson na yule wa IKEA aitwaye Ingvar Kamgrad kamwe hawakukanyaga chuo kikuu?
Msingi wa Ujasiriamali kinaangazia nguvu ya Ujasiriamali, papo hapo kikitambua madhaifu yake.Kinajadili majaribio (ambayo mara nyingi hushindwa) ya serikali ya kutaka kuuongoza. Na kinatamka kwa ufasha namna ya kuufanya ujasiriamali kuchukua mkondo mkuu wa uchumi na siasa.
Zaidi ya yote, kinaonesha thamani na kutoa utangulizi wa msingi wa maana ya ujasirimali, kwa nini tunauhitaji, na jinsi gani tunaweza kuuhamasisha.