Ukosefu wa Usawa wa Kiuchumi
Endapo ungaliweza kufanya maskini wa dunia kuwa tajiri mara mbili zaidi – lakini papo hapo kufanya matajiri wa dunia kuwa maskini mara mbili zaidi – je, ugefanya hivyo?
Swali hili la aina yake ndilo msingi wa kitabu hiki “Ukosefu wa Usawa wa Kiuchumi.”
Ukosefu wa usawa umelaumiwa kwa mambo mengi, kuanzia matarajio ya chini ya umri wa kuishi, elimu duni, vurugu za kisiasa, hadi ongezeko la visa vya kujiua, unene uliopitiliza, magonjwa ya akili na mauaji. Madai kwamba matajiri wakubwa zaidi, yaani asilimia moja (1%) tu ya watu duniani kumiliki asilimia arobaini (40%) ya utajiri wote wa sayari hii – na kwamba wanaendelea kutajirika zaidi – hutumika kila wakati kuonyesha ubaya wa ukosefu wa usawa.
Mwandishi Eamonn Butler anaupinga mtazamo huu unaosikika sana. Anahoji endapo tunauliza maswali sahihi. Je, tofauti za kimaisha hazitokani na watu kutofanana katika uwezo, chaguzi, hatari wanazokabili au hata bahati? Kwani usawa ndio lengo kuu la maisha?
Butler anatualika kushughulikia matatizo halisi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yanayoathiri maisha ya watu maskini. Anaona kuboresha elimu ni vema zaidi katika kuleta usawa badala ya kufanya mgawanyo wowote mpya wa kipato.
Pia anatoa hoja kwamba kujikita sana katika ukosefu wa usawa kunafanya tupoteze dira ya kufikia kilicho muhimu kwetu: si kwamba kila mtu anapaswa kuwa sawa, bali kila mtu apate fursa ya kiwango kinachofaa cha maisha.
Ukosoaji huu mfupi wa wazi una mchango wa kuvutia na wenye manufaa kwenye mjadala wa mada mojawapo inayovuta hisia kali katika karne ya 21. Vitabu vitatu vya awali katika mfululizo huu – Msingi wa Ujasiriamali, Demokrasia na Biashara & Utandawazi – vinapatikana kupitia www.libertysparks.org, au kwa wauzaji wa mtandaoni.
Kiswahili.
Ukosefu wa Usawa wa Kiuchumi
English Version.