Biashara za mipakani zinavyoongeza chachu katika uchumi
Na Penina Malundo
BIASHARA ni shughuli au mchakato wa kununua na kuuza mali au vitu na inaweza kufanywa na mtu binafsi au kwa ushirikiano au na jamii au nchi kwa jumla.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya biashara na kampuni zinazoanza hufa ndani ya mwaka wa kwanza tangu kuanzishwa kwake na katika hizo asilimia 20 zilizobaki asilimia 10 hufa ndani ya miaka mitano tangu kuanzishwa.
Biashara ndogo ndogo na za kati,zinawakilisha karibu asilimia 90 ya biashara za kimataifa, zaidi ya asilimia 60 ya ajira na nusu ya pato la taifa duniani kote na ndio tegemeo la kiuchumi la jamii kote ulimwenguni.
Moja ya Changamoto zinazowakwamisha ufanyaji wa biashara katika nchi nyingi za afrika hasa maeneo ya mipakani ni uwepo wa vikwazo vingi nvisivyokuw na tija.
Na hili changamoto hizo ziweze kuondolewa ni vema nchi hizo za Afrika ikiwemo Tanzania kuendelea kuona kuna umuhimu wa kuondoa vikwazo na kushirikiana na sekta binafsi katika kumaliza vikwazo hivyo.
Soko la Afrika Mashariki ni kubwa na Tanzania inazalisha vitu vingi ambavyo nchi jirani hawazalishi hivyo hiyo pia ni fursa moja wapo kwa wajasiramali hao.
Naibu Waziri,Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Exaud Kigahe anasema miaka ya sasa imekuwa ni rahisi kwa Mwafrika kufanya biashara ulaya kuliko kufanya nchi za Afrika.
’’Si jambo jema kwa afya na maendeleo ya biashara katikanchi zetu ufike wakati tuamue kwamba mtu wa kwanza kufanya naye biashara kirahisi ni yule wa karibu na nchi yako,’’anasema
Anasema katika kutatua changamoto za kibiashara,serikali ya Tanzania imeweza kupunguza vikwazo 30 kati ya vikwazo 60 za kikodi katikampakawakenya.
’’Lengo la kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara wa nchi zote mbili na nyingine Afrika Mashariki,’’ anasema na kuongeza.
‘’Tanzania tunataka kushirikiana na majirani zetu katika shughuli za kiuchumi, ili hatuwezi kufanikiwa kama hatutapunguza vikwazo kwenye mipaka na ndio maana serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepunguza vikwazo 30 kwa wenzetu wa Kenya,’’ anasema.
Mkurugenzi wa Shirika la Liberty Sparks, Evans Exaud akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uhuru wa kiuchumi iliyoandaliwa na shirika lisilola kiserikali lililojikita katika elimu na utafiti la Liberty Sparks. (Na Mpigapicha Wetu)
Kwa Upande wake Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uhuru wa kiuchumi iliyoandaliwa na Shirika lisilola kiserikali lililojikita katika elimu na utafiti la Liberty Sparks anasema wafanyabiashara nchini wametakiwa kuendelea kujikita zaidi katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali na kuangalia fursa zingine za kibiashara ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mbwasi anasema Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika kuhakikisha inakuwa na uhuru wa kiuchumi kwa wananchi hivyo ni muhimu jamii na wafanyabiashara
kuendelea kuangalia fursa za kibiashara ili kuweza kujipatia kipato na kuondoa umaskini.
“Msingi huu wa uhuru wa kiuchumi unatokea kwenye Katiba ya nchi ambayo inaelekeza kwamba mwananchi atakuwa huru kujishughulisha na shughuli za uzalishaji ili aweze kujipatia kipato, ndio maana tunawaomba wafanyabiashara na jamii yote kwa ujumla kujikita katika uwekezaji na kuangalia fursa za kibiashara ili waweze kujikwamua kiuchumi,” anasema.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Liberty Sparks,Evans Exaud anasema ripoti hiyo ya uhuru wa kiuchumi imefanywa na Profesa Samwel
Wangwe kwa kushirikiana na Profesa Sauti Magai wote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitengo cha biashara.
Anasema ripoti hiyo imejikita katika mambo matano ambayo yanalenga zaidi kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuongeza na kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa uhuru wa kiuchumi hapa nchini.
“Kupitia ripoti hii sisi Liberty Sparks tumejikita zaidi katika mambo manne ambayo ni biashara za mipakani, upatikanaji wa haki, hatimiliki pamoja na mikopo, tumekuja na majibu ambayo kama yatachukuliwa na Serikali yataisaidia Tanzania kukua kiuchumi,” anasema Exaud.
Anasema Liberty sparks
inatambua mchango mkubwa wa serikali wa kuboresha mazingira rahisi na rafiki ya ufanyaji biasharapamoja na kutambua mchango mkubwa wa wadau kucochea maendeleo ya nchii na kutoa nafasi ya kufanya tathimini yavipaumbelevyaserakwa kulinganisha na nchi zilizofanikiwa.
Exaud anasema hakuna wakati katika historia ya mwanadamu biashara zimekuwa zikifanyikwa kwa ushindani kama sasa.
’’Yaani usitegemee kuanzisha biashara ambayo haina ushindani,ni ngumu sana kuanzisha biashara ambayo haijawahi kufanyika kabisa hapo kabla hivyo ni vema kujipanga,’’anasema.
Statement: A Peaceful, Freer and Prosperous Africa can Defeat Coups- African Think Tanks