
Ripoti ya Haki za Ardhi kwa Wanawake Tanzania 2023.
- Version
- Download 84
- File Size 4.87 MB
- File Count 1
- Create Date February 9, 2024
- Last Updated February 9, 2024
Ripoti ya Haki za Ardhi kwa Wanawake Tanzania 2023.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoendelea duniani, ambako hakuna usawa wa kijinsia kuhusiana na upatikanaji wa ardhi. Upatikanaji wa ardhi ni muhimu kwa kupambana na ubaguzi na kukabiliana na umaskini nchini Tanzania. Wanawake ambao wananyimwa haki ya kupata ardhi huwa na shida na kwa hali hiyo, huishia kukosa nguvu za kiuchumi. Utafiti kuhusu wanawake kupata ardhi ulifanyika Makete, Tanzania (Moyo, 2017). Matokeo yalionyesha kuwa wanawake wengi wa vijijini hawajui kusoma na kuandika; hawajui haki zozote zilizopo na hawana rasilimali za kutosha kupigania haki zao na kwamba ushiriki wao katika taasisi za usimamizi wa ardhi ni mdogo.
Utafiti huo ulibainisha zaidi kuwa katika ngazi ya familia, mabinti na wanawake wananyimwa haki yoyote ya kumiliki ardhi, kupitia urithi kwa sababu ndugu zao wanaamini kuwa wataolewa na familia nyingine ambako huko watapata ardhi. Kwa hiyo, kuna changamoto nyingi katika kutambua haki za mali za wanawake nchini Tanzania. Hii ni pamoja na mfumo pacha wa haki za umiliki mali; umiliki wa kimila unafanya kazi sambamba na umiliki wa kisheria; maarifa duni juu ya haki za mali za wanawake na wanaume; mitazamo hasi juu ya ushawishi wa wanawake, nafasi, uwezo na sifa; mila zilizopitwa na wakati; masilahi ya zamani na yanayokinzana katika sheria; na ukosefu wa uwezo wa kisheria (uwezeshaji) juu ya haki za mali.
Pakua ripoti hii kujua zaidi.
Attached Files
File | Action |
---|---|
Haki za Ardhi Kwa Wanawake Tanzania, 2023 (1).pdf | Download |