Biashara na Utandawazi
- Version
- Download 500
- File Size 903.75 KB
- File Count 1
- Create Date April 2, 2022
- Last Updated April 2, 2022
Biashara na Utandawazi
KUHUSU MWANDISHI WA KITABU HIKI
Eamonn Butler ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Adam Smith, mojawapo kati ya taasisi andamizi za washauri mabingwa wa sera duniani. Ni msomi mwenye shahada katika fani za uchumi na saikolojia, shahada ya uzamivu katika falsafa na shahada ya uzamivu ya heshima ya DLitt. Katikati ya miaka ya 1970
alifanya kazi mjini Washington katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, na alifundisha falsafa katika Chuo cha Hillsdale, Michigan, kabla ya kurejea Uingereza ambapo alisaidia kuasisi Taasisi ya Adam Smith. Akiwa ni mshindi wa zamani wa Medali ya Uhuru inayotolewa na Freedom's Foundation of
Valley Forge na Tuzo ya National Free Enterprise ya Uingereza; filamu yake ya Siri za Magna Carta ilishinda tuzo katika Tamasha la Filamu la Anthem, na kitabu chake cha Taasisi za Jamii Huria kilishinda Tuzo ya Vitabu ya Fisher.
Eamonn ni mwandishi wa machapisho juu ya wachumi na wanazuoni ambao ni watangulizi wake: Adam Smith, Milton Friedman, F. A. Hayek na Ludwig von Mises. Pia ni miongoni mwa waandishi wa awali kutoa machapisho juu ya mwelekeo wa kisasa wa mabadiliko, uchaguzi wa umma, ubepari, demokrasia,
Fikra za Kichumi za Wanazuoni wa Kiaustria na wanazuoni mashuhuri wenye mwelekeo unaopendelea mabadiliko, pamoja na Mlimbikizo wa Utajiri wa Mataifa na Kitabu Bora Kabisa Kuhusu Soko. Vilevile ni mwandishi mshiriki wa Karne Arobaini za Udhibiti wa Ujira na Bei, na mfululizo wa vitabu juu ya akili na upimaji wa kiwango cha akili. Ni mchangiaji wa mara kwa mara katika uchapishaji, utangazaji na majukwaa ya mtandaoni.
Attached Files
File | |
---|---|
Biashara na Utandawazi.pdf |