Adam Smith Mtangulizi
- Version
- Download 430
- File Size 1.10 MB
- File Count 1
- Create Date November 10, 2021
- Last Updated November 10, 2021
Adam Smith Mtangulizi
Licha ya umashuhuri wake,bado kuna umbumbumbu ulioenea sanakuhusu mchango mkubwa wa Adam Smith katika uchumi, siasa na falsafa. Katika kitabu cha Adam Smith - Mtangulizi, Eamonn Butler anatoa utangulizi wa kuaminika wa maisha na kazi za “muasisi wa uchumi”.
Mwandishi huyu anafanya uchanganuzi siyo tu wa kitabu cha Utajiri wa Mataifa, chenye umaizi wa Adam Smith juu ya shughuli za biashara na mgawanyo wa nguvukazi, bali pia kazi zisizojulikana sana za Smith, mfano kitabu cha Nadharia za Maono ya kimaadili, mihadhara yake na maandishi yake juu ya historia ya sayansi. Butler, hata hivyo, siyo tu anatoa muhtasari unaojitosheleza wa mafanikio ya kiakili ya Adam Smith bali anatoa ufupisho wenye habari nyingi katika maelezo machache.
Japokuwa waandishi wa kabla yake waliweza pia kutafiti masuala ya kiuchumi, ni dhahiri kwamba wigo wa uchunguzi wa Smith ulikuwa wa ajabu usio na kifani. Anapoonesha jinsi kupiga hatua kiuchumi kuna uhusiano na asili ya mwanadamu pamoja na mabadiliko ya kijamii anatupatia uelewa mpya kabisa wa jinsi jamii ya wanadamu inavyofanya kazi. Kwa hakika alikuwa mtangulizi wa waandishi bora kama Hayek na Popper. Ukweli ni kwamba, katika mazingira yetu ya uzingativu duni wa utawala bora, vikwazo vya kufanya biashara na uingiliaji kati wa mamlaka za kiutawala, hoja za Smith zinaendelea kuwa za maana kwa watunga sera wa siku hizi.
Adam Smith - Mtangulizi, kinajumuisha dibaji iliyoandikwa na Sir Alan Peacock, pamoja na utangulizi wa Gavin Kenndy na maoni ya Craig Smith.
Toleo hili la Kiswahili limetafsiriwa na Elias Mutani.Kuchapishwa na Taasisi ya Liberty Sparks chini ya uangalizi wa Mkurugenzi wake Evans Exaud.
Attached Files
File | Action |
---|---|
Adam_Smith .pdf | Download |