Kodi na Tozo Zinazojirudia: Jinsi Sera za Fedha Zinavyoathiri Upatikanaji wa Masoko ya Kilimo

Liberty Sparks inakualika kushiriki katika mjadala wa kitaifa kuhusu changamoto za kodi, ushuru na tozo zinazojirudia katika sekta ya kilimo, na namna sera za fedha za Serikali zinavyoathiri upatikanaji wa masoko kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo nchini Tanzania.

Mjadala huu unalenga kukusanya maoni, uzoefu na mapendekezo ya wadau wa sekta ya kilimo kuhusu masuala muhimu yanayoathiri uhuru wa kufanya biashara na upanuzi wa masoko, ikiwemo:

  • vikwazo vya kisheria na kiutawala

  • gharama za kufanya biashara katika mnyororo wa thamani wa kilimo;

  • ushindani katika masoko ya mazao ya kilimo;

  • masuala ya utawala bora na uwajibikaji wa taasisi husika; na

  • vipaumbele vya maboresho ya sera na mifumo ya kodi na tozo.

Matokeo ya mjadala huu yatatumika kama mchango muhimu katika kuandaa Ripoti ya Ukaguzi wa Uhuru wa Kiuchumi (Economic Freedom Audit Report) ya Liberty Sparks, inayolenga kubaini maeneo ya sera na mifumo ya kiutawala yanayohitaji maboresho ili kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza upatikanaji wa masoko, na kuchochea ukuaji jumuishi katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Jisajili sasa kushiriki na kutoa mchango wako katika kuimarisha sera na mazingira ya biashara ya kilimo nchini.

Venue Info

Protea Hotel Dar es Salaam Courtyard, Barack Obama Drive, Dar es Salaam, Tanzania

View on Map
  • Date : February 10, 2026
  • Time : 11:34 am - 12:34 pm (Africa/Dar_es_Salaam)
  • Venue : Protea Hotel Dar es Salaam Courtyard, Barack Obama Drive, Dar es Salaam, Tanzania

Related Events

Conference Economy
PSSSF Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania

UHURU BUSINESS FORUM