Dar es Salaam. Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2019 inaonyesha kwa ujumla maendeleo ya binadamu nchini kwa mwaka 2018 yalirudi nyuma kwa asilimia 24.9, ikilinganishwa na mwaka 2017. Uchambuzi katika ripoti hiyo umezingatia hali ya kutokuwapo usawa katika mazingira ya kuzaliwa mtoto, katika kipato, katika elimu na katika tofauti kwa wenye mali na wasiokuwa nazo. Pamoja na hali hiyo, Tanzania bado inaonekana kuwa juu ya makadirio ya jumla katika ukanda wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (asilimia 30.5) na kidunia (asilimia 31.1).

Ripoti hiyo ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) iliyozinduliwa Desemba 18, mwaka jana ikiwa na jina la “Mtizamo wa Zaidi ya Pato, Zaidi ya Wastani, Zaidi ya Mahitaji ya Leo: Tofauti za Kijamii na Kiuchuni Katika Karne ya 21”, inahusisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN). “Maendeleo yamerudi nyuma kutokana na ukuaji wa uchumi kutokuwa jumuishi katika sekta zinazohusisha maisha ya Watanzania wengi,” alisema Dk Abel Kinyondo wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). “Katika miongo miwili iliyopita, uchumi umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 7, lakini unahusisha sekta zisizokuwa na ajira ya Watanzania wengi. Ndio maana unasikia wanalalamika uchumi unakuwaje wakati hakuna pesa. Matokeo yake tabaka la maskini na tajiri linaongezeka.

Other related News

WHO CONSULTATIVE PAPER

Summary Already, the alcohol industry today faces relatively many restrictions regarding availability and rules on consumption. Different countries have set a minimum age, opening and closing hours of pubs and liquor shops, various measures in drink and driving...

read more

Tanzania joins middle-income status ahead of schedule

The World Bank (WB) upgraded Tanzania’s country classification by income level from low income to lower-middle income in 2020-21. The WB assigns the world’s economies to four income groups—low, lower-middle, upper-middle, and high-income countries, based on their GNI...

read more
(Visited 29 times, 1 visits today)
Translate »